Leo Katika Magazeti ya Kimataifa

Mukhtasari wa Magazeti ya Kimataifa 08.06.2021

1653665
Leo Katika Magazeti ya Kimataifa

Le Soir: Maafisa wachache waliochaguliwa wa Mji Mkuu wa Brussels, Ubelgiji  walitangaza kuwa kutoka 9 Juni haitakuwa lazima tena kuvaa barakoa nje, isipokuwa kwenye barabara zilizojaa watu na sehemu za ununuzi.

Le Monde: Covid-19 Ulimwenguni : Uhispania inafungua tena mipaka yake kwa watalii waliopewa chanjo.

France 24: Kulingana na utafiti, karibu robo ya maafisa wa polisi wana "mawazo ya kujiua."

 

Eldustour: Lebanon: "Waandamanaji walifunga barabara ili kupinga ukataji wa mafuta na umeme."

Elquds Elarabi: Maonyo ya upinzani wa Wapalestina yalisababisha jeshi kupeleka Iron Dome, na maandalizi ya Jerusalem yalilazimisha walowezi hao kughairi maandamano yao ya uchochezi.

Eldustour: Jumuiya ya Kiarabu imeonya Israel juu ya hatua yoyote ambayo itazidisha hali Jerusalem.

 

El País, Uhispania: Uhispania yazindua cheti cha dijitali kuweza kusafiri Ulaya.

La Vanguardia, Uhispania: Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sánchez na Rais wa Catalonia Pere Aragonès walikubaliana kuanza awamu mpya ya mazungumzo na makubaliano.

El Comercio, Peru: Bodi ya Kitaifa ya Uchaguzi ilitangaza kwamba asilimia 93.66 ya kura zilihesabiwa baada ya uchaguzi huko Peru, huku Pedro Castillo akipata asilimia 50.18 na Keiko Fujimori asilimia 49.82 ya kura.

 

Tagesschau.de: Umri wa kustaafu nchini Ujerumani unaweza kuwa 68. Inasemekana katika bunge kwamba ikiwa umri wa kustaafu sio 68, shida ya kiuchumi itakabiliwa.

Frankfurter Rundschau: Taasisi ya Robert Koch inaripoti kuwa kuna kesi chache na mpya za maambukizi ya corona (Covid-19) nchini Ujerumani.

Spiegel.de: (Kashfa ya barakoa ) Waziri Mkuu wa Ujerumani Angela Merkel anamtetea Waziri wa Afya Jens Spahn.

 

TASS: China imetangaza utayari wake wa kuimarisha mazungumzo na Shirikisho la Urusi juu ya suala la Rasi ya Korea.

RIA Novosti: Rais wa Marekani Joe Biden alimpiga simu na mwenzake wa Ukraine Vladimir Zelenski na akamwalika atembelee Washington msimu huu wa joto.

RBK: Ubalozi wa Urusi nchini Marekani umeelezea ushiriki wa Marekani katika Zoezi la Arctic Challenge Exercise  huko Scandinavia kama uchochezi.Habari Zinazohusiana