Leo Katika Magazeti ya Kimataifa

Mukhtasari wa Magazeti ya Kimataifa 07.06.2021

1652914
Leo Katika Magazeti ya Kimataifa

Al Quds Al Arabi: Waziri wa Mambo ya nje wa Israel Gabi Ashkenazi alimtahadharisha Waziri Mkuu wa mpito Benjamin Netanyahu dhidi ya uchochezi wa hali ya karibu na Msikiti wa Al-Aqsa

Al-Dustour (Jordan): Marekani inajali hali ya Jerusalem na uwezekano wa shambulizi jingine dhidi ya Gaza.

Al Jazeera: Bwawa la Nahda – Tahadhari kutoka Misri na Sudan zaongezeka. Jeshi la Ethiopia pia lilithibitisha kuwa liko tayari kujibu shambulizi lolote.

 

Der Standard (Austria): Serikali ya Urusi imepanga kukamilisha bomba la Nord Stream 2 mwishoni mwa mwaka.

Frankfurter Allgemeine Zeitung: Uchaguzi wa bunge la serikali ya jimbo la Saxony-Anhalt - Christian Democratic Union (CDU) ilishinda kwa tofauti kubwa dhidi ya chama cha Alternative nchini Ujerumani (AfD).

Spiegel.de: Fidia ya Corona - Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump alidai fidia ya dola trilioni 10 kwa China kutokana na janga la coronavirus

 

El País (Uhispania): Mazungumzo juu ya mageuzi ya "Sheria ya Usalama wa Raia" yalikwama. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Uhispania inasisitiza kurudi haraka kwa wahamiaji waliokamatwa mpakani, licha ya upinzani wa mshirika wa serikali Unidas Podemos.

El Universal (Mexico): Merikani (USA) iliipongeza Mexico kwa "kufanikisha mchakato wa uchaguzi".

El Comercio (Peru): Uchaguzi Mkuu nchini Peru: Keiko Fujimori alifikia asilimia 52.4; Pedro Castillo alipata kwa asilimia 47.5.

 

Le Parisien: Kwa upande wa uwekezaji wa kigeni, Ufaransa inaendelea kuwa nchi ya kuvutia zaidi barani Ulaya.

Le Monde: (Rais wa Ufaransa) Emmanuel Macron anataka kutumia fursa ya hali bora ya kiafya nchini kuanzisha tena "ustaarabu wa kisasa" wa nchi hiyo.

Le Figaro: Ufaransa kuwa mwenyeji wa mamia ya wafanyikazi wa Afghanistan walio katika hatari.

 

 Habari Zinazohusiana