Leo Katika Magazeti ya Kimataifa

Mukhtasari wa Magazeti ya Kimataifa 27.05.2021

1646543
Leo Katika Magazeti ya Kimataifa

El País (Uhispania): Nadharia ya ajali ya maabara huko Wuhan, China inaimarisha kama chanzo cha janga la corona (Covid-19).

Infobae (Argentina): Gavana wa Argentina ambaye hapo awali alichomwa dozi mbili za chanjo ya Sputnik V alikutwa na maambukizi ya Covid-19.

Telesur (Venezuela): Watu wengi wajeruhiwa na kuzuiliwa katika uvamizi mpya wa polisi nchini Colombia.

 

Deutsche Welle: Mjadala wa chanjo ya Covid-19 kwa watoto na vijana nchini Ujerumani.

Tagesschau: Waziri Mkuu wa Ujerumani Angela Merkel ameamua kupanua vikwazo dhidi ya Belarus.

Welt.de: Uswisi Brexit: Uswizi imemaliza mazungumzo ya makubaliano ya mfumo na Jumuiya ya Ulaya (EU).

 

Elraya: Qatar imetenga msaada wa dola milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa Gaza.

Eldutour: Mfalme wa Jordan, Abdullah wa Pili, alisema katika mkutano wake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken kwamba, "Ukosefu wa suluhisho la kisiasa unasukuma kanda hiyo katika mvutano zaidi."

Elqudus Elarabi: Mwenyekiti wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas Ismail Haniyeh: "Tulituma ujumbe kwa Washington na Tel Aviv kwamba Jerusalem ni "mstari mwekundu" na kwamba tutaweka sheria za ushiriki."

 

Le Figaro: Covid-19: Virusi vya India vinaenea kote ulimwenguni, nchi zinajiandaa baada ya mzozo wa janga.

France 24: (Rais wa Ufaransa) Emmanuel Macron atembelea Rwanda; analenga kurekebisha uhusiano kati ya nchi hizi mbili.

France 24: Uswizi ilikomesha mazungumzo juu ya uhusiano wake na EU.

 

REGNUM News Agency: Waziri wa Mambo ya nje wa Ukraine Dmitriy Kuleba aliahidi kupambana hadi mwisho na mradi wa bomba la gesi asilia la Nord Stream-2.

Kommersant: Msemaji wa Idara ya Ulinzi ya Marekani John Kirby alisema Pentagon haitazami Urusi kama adui.

RIA Novosti: Wizara ya Ulinzi ya Armenia ilitangaza kwamba wanajeshi sita wa Armenia walichukuliwa wafungwa katika mkoa wa Gegharkunik kwenye mpaka wa Azerbaijan.Habari Zinazohusiana