Leo Katika Magazeti ya Kimataifa

Mukhtasari wa Magazeti ya Kimataifa 06.05.2021

1634959
Leo Katika Magazeti ya Kimataifa

zdf.de: Kifurushi cha euro bilioni 2 kilichoandaliwa kusaidia wanafunzi ambao walibaki nyuma katika madarasa yao kwa sababu ya hatua za corona nchini Ujerumani kilikubaliwa na baraza la mawaziri.

Süddeutsche Zeitung: Mtandao wa kijamii wa Facebook umeamua kuendelea kupiga marufuku matumizi ya akaunti za mitandao ya kijamii za Rais wa zamani wa Marekani (USA) Donald Trump.

Welt.de: Robo ya raia wa Jumuiya ya Ulaya (EU) walipokea dozi ya kwanza ya chanjo.

 

Le Monda: Mwanamke aliyechomwa moto na mumewe katikati ya barabara huko Merignac nchini Ufaransa alikufa.

France 24: Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ambaye alitoa taarifa juu ya kumbukumbu ya miaka 200 ya kifo cha Napoleon (Mwanajeshi wa Ufaransa na mwanasiasa), alisema "Napoleon ni sehemu yetu."

Le Parisien: Afisa wa polisi alipigwa risasi na kuuawa huko Avignon, Ufaransa wakati wa operesheni ya dawa za kulevya.

 

Al-Quds Al-Arabi: Jumuiya ya Ulaya inaitaka Israel iache kupanua makazi yake katika maeneo ya uvamizi.

Al-Quds Al-Arabi: Libya .. Wajumbe kutoka eneo la mashariki walitembelea mji mkuu wa Tripoli na kumtaka Waziri Mkuu wa Libya Abdulhamid Dbeibeh kuharakisha ziara yake ya Benghazi.

Al Jazeera: Vyanzo vya kidiplomasia: "Pengo kubwa kati ya Tehran na Marekani limesimamisha maendeleo kwenye mazungumzo ya Vienna."

 

El Pais: (Uhispania) Kufuatia kutofaulu kwa vyama vya mrengo wa kushoto katika uchaguzi wa mapema wa wabunge uliofanyika Jumanne, Mei 4, chini ya utawala huru wa Madrid, wabunge wengine kutoka Chama cha Wafanyakazi cha Kijamaa cha Uhispania (PSOE) wametangaza kuwa wanaamini kufufua uchumi ili kubadili hali.

El Mundo: (Uhispania) Inatabiriwa kuwa Waziri wa Kazi Yolanda Díaz atakuwa kiongozi mpya wa chama baada ya kiongozi wa chama cha Podemos Pablo Iglesias kuacha siasa.

TeleSur: (Venezuela) Matukio ya ghasia yaendelea usiku kati ya vikosi vya usalama na waandamanaji huko Colombia, waandamanaji wengine wawili walifariki katika mji wa Pereira.

 

Lenta.ru: Ukraine iliishutumu Urusi kwa kutumia vibaya jukwaa la Umoja wa Mataifa.

TASS: Chanjo bora ya corona (Covid-19) ilichaguliwa katika Kongamano la Chanjo Ulimwenguni. Moderna ilizingatiwa kuwa chanjo bora.

Gazeta.ru: Wataalam wa Marekani wanadhani kuwa mkutano unaowezekana kati ya Rais wa Marekani Joe Biden na Rais wa Urusi Vladimir Putin unaweza kufanyika katika miji mikuu ya Jamhuri ya Czech, Iceland, Slovenia au Azerbaijan.Habari Zinazohusiana