Leo Katika Magazeti ya Kimataifa

Mukhtasari wa Magazeti ya Kimataifa 05.05.2021

1634201
Leo Katika Magazeti ya Kimataifa

Al-Jazeera (Televisheni ya Qatar): Rais Recep Tayyip Erdoğan na Mfalme Salman bin Abdulaziz wa Saudi Arabia waliwasiliana kwa njia ya simu. Uhusiano wa pande mbili ulijadiliwa katika mkutano huo.

al-Düstur (Jarida la Jordan): Mazungumzo ya kuweka mipaka ya baharini kati ya Lebanon na Israel yaanza tena.

al-Quds al-Arabi (Jarida la Kiarabu - Uingereza): Polisi Derek Chauvin nchini Marekani (USA) anadai kusikilizwa tena baada ya kupatikana na hatia ya kumuua George Floyd mwenye asili ya Kiafrika.

 

nex24.news: Teknolojia ya ulinzi - Uturuki imefanikisha majaribio ya roketi yake ya ulinzi wa anga HİSAR-A.

Deutsche Welle: Corona - Serikali ya Ujerumani imepitisha amri ya kutoa haki ya msingi kwa wale ambao wana chanjo ya corona na wale ambao waliugua na kupona ugonjwa huo.

 

El Mundo (Uhispania): Chama cha People’s Party (PP) kimefikia hatua ya kihistoria kwa mrengo wa kushoto. Kilishinda uchaguzi wa seriakli za mitaa katika jiji la Madrid.

El País (Uhispania): Pablo Iglesias, kiongozi wa Chama cha Unidas Podemos huko Uhispania, alitangaza kwamba aliacha siasa baada ya kushindwa kwa mrengo wa kushoto huko Madrid.

Telesur (Venezuela): Watu 19 walifariki katika maandamano ya kupinga marekebisho ya ushuru huko Colombia tangu Aprili 28.

 

Le Figaro: Covid-19: Mmoja kati ya watu wanne wa Ulaya walipewa chanjo kwa mara ya kwanza, Marekani iliongeza kasi ya kampeni yake ya chanjo.

Le Monde: Misri inathibitisha kuwa imenunua ndege 30 za kivita za Rafale kutoka Ufaransa.

France 24: Ufaransa inalenga kutoa chanjo ya Covid-19 kwa watu milioni 3 wiki hii.

 

RIA Novosti: Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alihimiza shinikizo kwa Urusi itekeleze majukumu yake ya kimataifa.

Lenta.ru: Pentagon (Idara ya Ulinzi ya Marekani) iliituhumu Urusi kwa kukiuka utaratibu wa utatuzi wa mgogoro wa Syria.

Gazeti la Kommesant: Kituo cha Utafiti cha Virolojia na Bioteknolojia cha "Veсtor" nchini Urusi chafanya majaribio ya kliniki ya chanjo ya "EpiVakKorona" itakayotengenezwa kwa dozi tatu.Habari Zinazohusiana