Leo Katika Magazeti ya Kimataifa

Mukhtasari wa Magazeti ya Kimataifa 27.04.2021

1628945
Leo Katika Magazeti ya Kimataifa

ard.de: Jumuiya ya Ulaya iliwasilisha kesi dhidi ya AstraZeneca kwa kukiuka makubaliano ya ununuzi wa chanjo (Covid-19).

Deutsche Welle: Rais wa Ujerumani na Ufaransa Frank-Walter Steinmeier na Emmanuel Macron, ambao walikutana huko Paris, walitoa ujumbe kwamba Ulaya, ambayo inapitia kipindi kigumu katika janga la corona, inapaswa kuwa na "umoja" haraka.

zdf.de: Idadi ya kesi za maambukizi ya virusi vya corona nchini India imefikia kiwango cha rekodi, na kufikia zaidi ya elfu 300 kwa siku tano mfululizo.

 

al-Quds al-Arabi (Jarida la Kiarabu - Uingereza): Ujerumani: Mtu mmoja mbaguzi aliyemshambulia kijana wa Syria kwenye treni asababisha mhemko.

al-Quds al-Arabi (Jarida la Kiarabu - Uingereza): Mfalme wa Saudi Arabia Salman bin Abdulaziz anamwalika Mtawala wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamed kutembelea Saudi Arabia.

al-Raye al-Qatariyye (Jarida la Qatar): Qatar inasaidia kuimarisha usalama na utulivu wa Saudi Arabia.

 

Le Parisien: Covid-19 Ufaransa: Udhibiti katika mipaka ya Ufaransa waongezeka kuzuia aina mpya ya virusi vya India.

Le Figaro: Ufaransa kutuma vifaa vya uzalishaji wa oksijeni nchini India.

Le Temps (Uswizi): Askari wa zamani waliostaafu waliamsha tena ari ya mapinduzi (hofu) huko Ufaransa.

 

La Vanguardia (Uhispania): Mkoa wa Catalonia unatarajia kupokea chanjo 400,000 au 450,000 kila siku saba kuanzia sasa.

ABC (Uhispania): Wanasayansi wa Peru wanashughulika na uchunguzi wa aina mpya ya virusi vya Covid-19 ambavyo vinadhaniwa kuonekana Peru au Chile, na "kuenea" kwa nchi zingine.

Prensa Latina (Cuba): Tume ya Uchunguzi ya Bunge inaanza uchunguzi leo kushughulikia uzembe unaowezekana kuwepo katika serikali ya Rais Jair Bolsonaro kufuatia mlipuko wa janga la Covid-19 nchini Brazil.

 

RIA Novosti: Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi ilitangaza kwamba watajiondoa kutoka kwa Mkataba wa Anga Wazi mwishoni mwa Mei.

TASS: Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alimweleza Rais wa Urusi Vladimir Putin juu ya mazungumzo yake na Rais wa Ukraine Vladimir Zelenski waliyofanya huko Paris.

Kommersant: Mfuko wa Uwekezaji wa moja kwa moja wa Urusi (RDIF) unapanga kusafirisha chanjo ya Sputnik V iliyoundwa dhidi ya corona kwenda India mnamo Mei 1.Habari Zinazohusiana