Leo Katika Magazeti ya Kimataifa

Mukhtasari wa Magazeti ya Kimataifa 25.01.2021

1570267
Leo Katika Magazeti ya Kimataifa

LeMonde: Mmoja wa watu wanaotafutwa zaidi duniani (Tse Chi Lop) kwa tuhuma za ulanguzi wa madawa ya kulevya huko Asia akamatwa nchini Uholanzi.

France 24: Simu ya kwanza kati ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Rais wa Marekani Joe Biden yafanyika baada ya kuingia madarakani.

Le Soir: Hofu juu ya aina mpya ya virusi vya corona (Covid-19) yatanda katika shule za Ubelgiji.

 

al-Quds al-Arabi (Gazeti la Kiarabu-Kiingereza): Balozi mpya wa Israeli awasili Washington na orodha ya madai atakayowasilisha kwa utawala wa Rais wa Marekani Joe Biden.

al-Raye al-Qatariyya (Gazeti la Qatar): Pongezi za kimataifa kwa juhudi za Qatar za kupambana na ufisadi.

ed-Düstur (Gazeti la Jordan): Serikali ya Yemen na wajumbe wa Houthis waanza mazungumzo Jordan.

 

El País (Uhispania): Uhispania inakabiliwa na kipindi kibaya zaidi cha wimbi la tatu kwa sababu ya matatizo ya aina mpya ya virusi vya corona vilivyotokea Uingereza.

El Universal (Mexico): Rais wa Mexico Lopez Obrador, kukutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa majadiliano juu ya usambazaji wa chanjo ya Sputnik V.

El Tiempo (Colombia): "Mabadiliko ya ghafla ya mwelekeo" kuzika enzi za Donald Trump huko Marekani: Rais mpya Joe Biden atia saini kanuni 30 za kumaliza mzozo uliopo sasa.

 

Deutsche Welle: Ankara na Athens kwenye meza ya mazungumzo tena baada ya miaka mitano.

Stuttgarter-Nachrichten.de: Mesut Özil, mmoja wa nyota wa soka ulimwenguni, ahamia rasmi kwa Fenerbahçe.

Tagesschau.de: Ujerumani inajiandaa kuwa nchi ya kwanza katika Jumuiya ya Ulaya kutumia kingamwili dhidi ya virusi vya corona.

 

Gazeta.ru News Site: Meli ya "Fortuna" yaanza tena ujenzi wa bomba la gesi asilia la "Nord Stream-2" nchini Denmark.

Gazeti la Izvestiya: Wakusanyaji fedha kinyume cha sheria kwa jina la misaada nchini Urusi wanaweza kutozwa faini.

Russia Today: Urusi yanyimwa haki ya kushiriki kwenye mikutano ya kujadili miradi iliyo chini ya Programu ya Kiamatifa ya Mwezini.Habari Zinazohusiana