Merkel na Leyen waunga mkono Uturuki

Waziri Mkuu wa Ujerumani Angela Merkel na Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya (EU) Ursula von der Leyen waunga mkono Uturuki kwenye suala la uhamiaji

1662794
Merkel na Leyen waunga mkono Uturuki

Waziri Mkuu wa Ujerumani Angela Merkel na Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya (EU) Ursula von der Leyen, walisema kuwa makubaliano ya uhamiaji kati ya EU na Uturuki ni muhimu na yanahitaji kuendelezwa zaidi.

Angela Merkel alifanya mkutano wa pamoja na waandishi wa habari na von der Leyen huko Berlin, mji mkuu wa Ujerumani.

Akiashiria kwamba Uturuki inahifadhi idadi kubwa ya wakimbizi, Merkel alisema,

"Makubaliano hayo ni muhimu na yanapaswa kuendelezwa zaidi. Uturuki inafanya kazi nzuri kupokea wakimbizi milioni 3.7 wa Syria. Uturuki inastahili msaada wetu."

Waziri Mkuu wa Ujerumani pia alisema kuwa suala la Umoja wa Forodha litajadiliwa katika Mkutano wa EU utakaofanyika tarehe 24-25 Juni.

Rais wa Tume ya EU von der Leyen pia alieleza kuwa walifanya mikutano mingi na Uturuki katika siku za hivi karibuni na kusema,

"Mara ya mwisho nilikutana na Rais Recep Tayyip Erdoğan jana. Hali ya hewa, umoja wa forodha na makubaliano ya uhamiaji yatajadiliwa katika Mkutano wa EU."

Akizungumzia wakimbizi wa Syria ambao wamekuwa Uturuki kwa karibu miaka 10, von der Leyen pia alisema,

"Jambo muhimu hapa ni kwamba tunaunga mkono Uturuki. Kuna wakimbizi milioni 3.7 wa Syria nchini Uturuki. Watu huko wanapaswa kuwa na mtazamo mzuri. Hii ni muhimu kwetu. Nitaleta suala hili katika Baraza."Habari Zinazohusiana