EU kununua dozi milioni 150 za chanjo ya Moderna

Jumuiya ya Ulaya (EU) yatangaza kuagiza dozi za ziada milioni 150 za chanjo iliyozalishwa na Moderna dhidi ya corona (Covid-19)

1662791
EU kununua dozi milioni 150 za chanjo ya Moderna

Jumuiya ya Ulaya (EU) itapokea dozi za ziada milioni 150 za chanjo iliyozalishwa na Moderna dhidi ya corona (Covid-19).

Tume ya EU imetangaza kuwa chaguo la kuchukua dozi za ziada limeamilishwa katika mfumo wa makubaliano ya pili ya ununuzi wa chanjo yaliyosainiwa na Moderna mnamo Februari.

Katika taarifa hiyo, ilibainika kuwa Moderna itatoa dozi milioni 150 za chanjo ya ziada kwa nchi wanachama wa EU mwaka 2022.

Kwa upande mwingine, EU haikutoa maelezo kuhusu bei ya chanjo kwa sababu ya usiri wa kibiashara.

EU ilisaini mkataba wa kwanza na Moderna kutoa dozi milioni 160 mnamo Novemba, na mkataba wa pili mnamo Februari kwa ununuzi wa jumla ya dozi milioni 300.

Hadi kufikia sasa, EU imeweza kusaini mkataba wa kupokea dozi bilioni 2.4 za chanjo ya BioNTech-Pfizer, dozi milioni 400 za AstraZeneca, dozi milioni 300 za Sanofi-GSK, dozi milioni 400 za Johnson & Johnson, dozi milioni 405 za CureVac na dozi milioni 460 za Moderna.

Kwa sasa, chanjo zinazozalishwa na kampuni za BioNTech-Pfizer, Moderna, AstraZeneca na Johnson & Johnson zimepokea idhini ya matumizi katika nchi za  EU.Habari Zinazohusiana