Guterres ateuliwa tena kama Katibu Mkuu wa UN

Antonio Guterres kuendelea kuhudumu kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) baada ya kuteuliwa tena

1660842
Guterres ateuliwa tena kama Katibu Mkuu wa UN

Antonio Guterres ameteuliwa tena kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) kuhudumu kwa muhula mwingine wa miaka 5.

Guterres, ambaye aliteuliwa na nchi yake ya Ureno na kuidhinishwa kama mgombea na Baraza la Usalama la UN, alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa UN kwa mara ya pili katika Mkutano Mkuu wa UN wa wanachama 193.

Muhula wa pili wa Guterres, ambaye bado ni Katibu Mkuu wa UN, utaanza rasmi tarehe 1 Januari 2022.

Makatibu Wakuu wa UN huchaguliwa kila baada ya kipindi cha miaka mitano.Habari Zinazohusiana