Kim Jong Un azungumzia hatari ya uhaba wa chakula Korea Kaskazini

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un ameonya kuwa hali ya chakula nchini humo "inatia wasiwasi"

1659215
Kim Jong Un azungumzia hatari ya uhaba wa chakula Korea Kaskazini

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un ameonya kuwa hali ya chakula nchini humo "inatia wasiwasi".

Akizungumza kwenye mkutano wa jana wa Kamati Kuu ya Chama Tawala cha Wafanyakazi, Kim alitaka mazungumzo na jamii ya kimataifa juu ya jinsi Korea Kaskazini inapaswa kukabiliana na "hali ya sasa ya kimataifa", shirika rasmi la habari la Korea Kaskazini KCNA liliripoti.

Kim hakutaja wazi Marekani na jirani yake wa Kusini katika mazunguzmo hayo.

Akisisitiza kuwa vizuizi vilivyotumika ndani ya wigo wa corona na majanga ya mafuriko mnamo 2020 yameathiri uchumi vibaya, Kim alionya juu ya uhaba wa chakula.

Kim amesema hali ya chakula nchini "inatia wasiwasi" na akahimiza mamlaka kuchukua hatua kuongeza uzalishaji wa kilimo.

Kwa kuongezea, Kim amesema kuwa wataendelea kutekeleza hatua za kupambana na janga licha ya ugumu wa kiuchumi.Habari Zinazohusiana