Merkel: ''Njia ya kujinasua kutokana na janga la Covid-19 ni chanjo''

Angela Merkel asisitiza umuhimu wa usambazaji wa chanjo ya Covid-19 ili kumaliza janga la corona

1657053
Merkel: ''Njia ya kujinasua kutokana na janga la Covid-19 ni chanjo''

Waziri Mkuu wa Ujerumani Angela Merkel alisema kuwa njia ya kujinasua kutokana na janga la corona (Covid-19) ni chanjo.

Merkel alifanya mkutano na waandishi wa habari siku ya mwisho ya Mkutano wa G7, uliofanyika Carbis Bay huko Cornwall, Uingereza.

Akibainisha kwamba walikubaliana kuwa janga hilo linaweza kushindwa kwa mapambano ya ulimwengu, Waziri Mkuu wa Ujerumani alisema kwamba walijadili juu ya usambazaji wa chanjo ya Covid-19 kwa nchi zinazoendelea.

Merkel alisema,

"Njia ya kujinasua kutokana na janga hilo ni chanjo. Tulijadili kwa kina kwamba tunahitaji kuhakikisha kila mtu anapata chanjo."

Akiashiria kwamba lengo la nchi za G7 kusambaza jumla ya dozi bilioni 2.3 za chanjo kwa nchi zinazoendelea ifikapo mwisho wa 2022 ni ishara njema, Merkel alisisitiza kuwa Ujerumani itachangia pakubwa suala hili.

Akiashiria kwamba ni muhimu kusaidia uzalishaji wa chanjo ulimwenguni, Merkel pia alisema,

"Tunataka chanjo isizalishwe Ulaya au Asia pekee, bali pia barani Afrika. Kampuni ya BioNTech inafanya kazi katika suala hili. Kampuni zingine pia zinashughulika."

Waziri Mkuu wa Ujerumani alifahamisha kuwa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) linapaswa kuimarishwa zaidi ili kuzuia magonjwa ya milipuko ya baadaye.Habari Zinazohusiana