EU yaidhinisha cheti cha chanjo ya Covid-19

Nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU) zaidhinisha aina mpya ya cheti cha chanjo ya corona (Covid-19)

1656380
EU yaidhinisha cheti cha chanjo ya Covid-19

Nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU) wameidhinisha aina mpya ya cheti cha chanjo ya corona (Covid-19) kitakachotumiwa katika safari ndani ya mipaka ya Muungano.

Baraza la Ulaya lilitangaza kuwa nchi wanachama wameidhinisha kanuni inayoitwa "Cheti cha EU Digital COVID". Hivyo basi, cheti cha chanjo cha EU kitakachotumika katika usafiri kitaanza rasmi mnamo 1 Julai.

Cheti cha chanjo kitakuwa bure, na kitatolewa kwa mfumo wa karatasi au fomu ya dijitali.

Ili kuzuia ubaguzi, watu ambao hawajapewa chanjo pia wataweza kukabidhiwa cheti hicho.

Cheti cha chanjo kitakuwa na maelezo yanayoonyesha iwapo mtu amepewa chanjo ya Covid-19, sehemu aliyopewa na aina ya chanjo iliyotumika, wale ambao wamepona ugonjwa huo na kuhusu urejesho wa wale ambao wana kiwango kikubwa cha kingamwili, pamoja na matokeo ya vipimo vya Covid-19.

Wamiliki wa cheti hawatakumbwa na vizuizi kama vile upimaji wa ziada au karantini hasa kwa wale watu ambao wamepokea chanjo zilizoidhinishwa za Covid-19 katika EU ndani ya wiki 2 za mwisho tangu kufanyiwa vipimo.

Katika hali zinazohitajika, kama vile kulinda afya ya umma, nchi zinaweza kuchukua hatua zaidi.

Cheti cha chanjo kitakuwa halali katika nchi zote za EU na vile vile Iceland, Liechtenstein, Norway na Uswizi.

Cheti kinaweza kutolewa kwa raia wa EU, familia zao bila kujali utaifa, na pia wakaazi wa EU pamoja na raia wasio wa EU na wageni walio na haki ya kusafiri kwenda nchi zingine za EU.

EU tayari imeidhinisha chanjo zinazozalishwa na BioNTech-Pfizer, Moderna, AstraZeneca na Johnson and Johnson.Habari Zinazohusiana