Chanjo ya Sinovav yaidhinishwa kwa watoto

China yaidhinisha matumizi ya chanjo ya Sinovac kwa watoto wenye umri wa kati ya miaka 3-17

1652366
Chanjo ya Sinovav yaidhinishwa kwa watoto

Chanjo ya Sinovac imeidhinishwa kutumiwa kwa watoto nchini China.

Kufuatia uamuzi huo, chanjo hiyo inaweza kutolewa kwa watoto wenye umri wa kati ya miaka 3-17.

Matumizi ya chanjo ya corona inayozalishwa na kampuni ya Kichina ya Sinovac imepewa idhini kwa ajili ya watoto nchini China.

Taarifa hiyo ilitoka kwa mkurugenzi mkuu wa Sinovac (Mkurugenzi Mtendaji), Yin Weidong.

Yin alisema kuwa walipokea idhini kutoka kwa Utaratibu wa Pamoja wa Baraza la Utawala wa China la Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa.

Bado haijulikani ni lini chanjo hiyo itaanza kutumika kwa watoto wenye umri wa kati ya miaka 3-17.

Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) liliidhinisha utumiaji wa dharura wa chanjo mpya ya Sinovac iliyotengenezwa na China mnamo Juni 1.

Shirika la Dawa la Ulaya liliidhinisha utumiaji wa chanjo ya Biontech / Pfizer katika kikundi watoto wenye umri wa kati ya miaka 12-15.Habari Zinazohusiana