Silaha kutolewa kama zawadi nchini Marekani

Usambazaji wa chanjo

1650271
Silaha kutolewa kama zawadi nchini Marekani

Silaha zitatolewa kama zawadi katika kampeni iliyoandaliwa kutangaza na kuhamasisha utumiaji wa chanjo hiyo katika jimbo la West Virginia huko Marekani.

Gavana wa West Virginia Jim Justice alitangaza kuwa katika bahati nasibu ya motisha ya chanjo, ambayo itafanyika Siku ya Baba na ambayo itajumuisha pesa ya tuzo ya $ 1 milioni, mikopo kwa ajili ya masomo, malori yenye vifaa maalum, kuingia bure katika mbuga za serikali, leseni za uwindaji na uvuvi, pamoja na silaha vitasambazwa kwa washiriki.

Bunduki 5 maalum na ambazo zimetajwa kuwa za uwindaji, zitapewa kwa wale watakaoshiriki kampeni hiyo na bahati nasibu.

Kampeni nyingi za kushinda tuzo zimepangwa huko Marekani ili kubadilisha maoni ya watu kuhusu chanjo.

 Habari Zinazohusiana