Zawadi ya pesa kwa wanaochomwa chanjo Marekani

Jimbo la California latangaza kugawa zawadi ya pesa kwa watu wanaokubali kuchomwa chanjo ya Covid-19 Marekani

1647704
Zawadi ya pesa kwa wanaochomwa chanjo Marekani

Zawadi ya dola milioni 116.5 kwa ujumla itasambazwa katika jimbo la California nchini Marekani (USA) ili kuhamasisha umma kuwa kukubali kupewa chanjo ya corona (Covid-19).

Gavana wa California Gavin Newsom alitangaza kuwa huko California, ambapo zaidi ya watu milioni 20 wamechomwa chanjo, watapewa zawadi ya pesa kuanzia Juni 4.

Katika muktadha huu, Newsom alibaini kuwa watasambaza jumla ya dola milioni 116.5 ndani ya wigo wa zawadi itakayojumuisha cheki ya dola milioni 1.5 kwa watu 10, dola 50,000 kwa watu 30, na dola 50 kwa watu milioni 2.

Kwa kutaka kutimiza lengo la kutoa chanjo kwa asilimia 70 ya idadi ya watu ifikapo katikati ya mwezi Juni ili kupunguza hatua za Covid-19, Newsom pia alisema kuwa rasilimali nyingi zimetengwa zaidi ya majimbo mengine huko Marekani ili kuharakisha utekelezaji wa mchakato wa chanjo.

Maafisa walibaini kuwa chanzo cha zawadi zitakazogawanywa kwa umma zitatengwa kutoka kwenye bajeti ya serikali ya misaada ya janga hilo.Habari Zinazohusiana