Chanjo yapunguza hatari ya maambukizi na vifo

Italia yadhihirisha kuwa chanjo ya Covid-19 yapunguza hatari ya maambukizi na vifo

1640348
Chanjo yapunguza hatari ya maambukizi na vifo

Chanjo zilizotengenezwa dhidi ya corona (Covid-19) zilibainika kuwa hupunguza hatari ya kuugua, kulazwa hospitalini na kufariki.

Wizara ya Afya ya Italia na Taasisi ya Afya ya Juu ya Italia (ISS) ilichapisha matokeo ya utafiti wa pamoja juu ya watu milioni 13.7 ambao walipokea chanjo ya Covid-19 katika kipindi cha kampeni ya chanjo iliyoendelezwa nchini humo kuanzia Desemba 27, 2020 hadi Mei 3, 2021.

Utafiti huo ulionyesha kuwa hatari ya kifo kutokana na Covid-19 ilishuka chini kwa asilimia 95 ndani ya siku 35 baada ya dozi ya kwanza ya chanjo kutolewa.

Ikilinganishwa na wale ambao hawajapewa chanjo, hatari ya kuambukizwa imepunguzwa kwa asilimia 80 na hatari ya kulazwa hospitalini imepunguzwa kwa asilimia 90 kwa wale ambao wamepewa chanjo.

Ilielezwa kuwa ufanisi wa chanjo hizo ulikuwa sawa kwa wanawake na wanaume wa vikundi tofauti vya umri.

Nchini Italia, chanjo 4 tofauti sasa zinatumika katika vita dhidi ya mlipuko wa Covid-19: Pfizer / BioNTech, Moderna, Johnson & Johnsan na Oxford / AstraZeneca.

Katika nchi hiyo ambayo kampeni ya chanjo dhidi ya Covid-19 ilianza mnamo Desemba 27, 2020, watu milioni 26 elfu 867 na 179 wamepewa chanjo hadi sasa.

Dozi ya pili ya chanjo ilitolewa kwa watu milioni 8 elfu  435 na 227 kati yao.Habari Zinazohusiana