Waziri Mkuu wa Malaysia awasiliana na mkuu wa Hamas

Waziri Mkuu wa Malaysia Muhyiddin Yasin awasiliana na Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas Ismail Heniyye

1639948
Waziri Mkuu wa Malaysia awasiliana na mkuu wa Hamas

Waziri Mkuu wa Malaysia Muhyiddin Yasin aliwasiliana na Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas Ismail Heniyye juu ya mashambulizi ya Israel dhidi ya Wapalestina huko Jerusalem Mashariki na Gaza.

Rais wa Shirika la Utamaduni la Palestina (PCOM) Muslim Imran alitangaza kuwa wakati wa mazungumzo ya simu yaliyodumu kwa nusu saa kati ya viongozi hao wawili, Heniyye alimjulisha Muhyiddin juu ya mashambulizi ya hivi karibuni ya Israel na majeruhi ya raia katika mkoa huo.

Imran alisema,

"Bwana Heniyye alielezea kuthamini kwake mshikamano wa Malaysia na watu wa Palestina hadi sasa, na alimfikishia Waziri Mkuu Muhyiddin msaada wa Malaysia kwa kushinikiza Israel kimataifa."

Akifahamisha kwamba Muhyiddin alisisitiza kuwa atatoa msaada kamili kwa Palestina, Imran pia alisema,

"Waziri Mkuu wa Malaysia atachukua msimamo dhidi ya Israel mbele ya Umoja wa Mataifa na Indonesia na Brunei, ambazo ni nchi za eneo hilo."

Imran pia alisema kuwa Muhyiddin alimwalika Heniyye nchini Malaysia baada ya hatari ya janga la Covid-19 kumalizika.Habari Zinazohusiana