Watu 139 wauawa katika mashambulizi ya Israel dhidi ya Palestina

Wapalestina 139 wauawa, zaidi ya 900 wamejruhiwa

1639813
Watu 139 wauawa katika mashambulizi ya Israel dhidi ya Palestina

Idadi ya watu waliopoteza maisha katika mashambulizi yanayofanywa na Israel dhidi ya Palestina imeongezeka hadi 139.

Wapalestina wengine kumi, wengi wao wakiwa watoto, wameuawa katika shambulizi la ndege za kivita za Israeli kwenye nyumba katika Kambi ya Wakimbizi ya Shati katika sehemu ya magharibi ya Gaza.

Tangu Mei 10, Wapalestina 139 wameuawa na Wapalestina 950 wamejeruhiwa katika shambulizi la vikosi vya Israel.

Wakati huo huo, ndege za kivita za Israeli zilishambulia maeneo ya kaskazini na kusini mwa Gaza, kulingana na habari kutoka vyanzo vya ndani vya eneo hilo.

Iliripotiwa kuwa ndege hizo zililenga nyadhifa za vikundi vya upinzani vya Wapalestina na nyumba kaskazini.

Kwenye upande wa kusini, ilirekodiwa kuwa nyumba ambayo ilipigwa bomu hapo awali ililengwa kwa mara ya pili na ndege, na pia mashambulizi  yalitekelezwa kwa risasi katika maeneo anuwai.

Ndege za kivita za Israel zilifanya mashambulizi kama 30 kaskazini mwa Gaza jana usiku.

Kama matokeo ya mashambulizi yaliyolengwa karibu na kurugenzi ya elimu, nyumba za raia na msikiti, umeme ulikatwa katika sehemu kubwa ya mkoa huo.

Kwa upande mwingine, Naibu Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas Salih al-Aruri amesema kuwa operesheni itakayozinduliwa kutoka ardhini huko Gaza itakuwa janga kwa Israeli na vita vitabadilisha usawa.

Akiongea na televisheni ya al-Aqsa ya Hamas juu ya habari kwamba Israeli ilianzisha operesheni ya ardhi huko Gaza hapo jana, Aruri alisema kuwa "vikosi vya upinzani vina nguvu ya kutosha kumshangaza adui (Israeli) na wana silaha zenye nguvu zaidi kuliko silaha zilizotumiwa kabla. "Habari Zinazohusiana