Marekani yasherehekea kuondolewa kwa sheria ya barakoa

Baraza la Wawakilishi lasherehekea baada ya uamuzi wa kuondoa sheria ya uvaaji barakoa na kuzingatia masafa baina ya watu

1639583
Marekani yasherehekea kuondolewa kwa sheria ya barakoa

Katika nchi ya Marekani, sherehe ilifanyika katika Baraza la Wawakilishi baada ya uamuzi wa kuondoa sheria ya uvaaji barakoa na kuzingatia masafa baina ya watu kwa wale waliopewa chanjo ya corona (Covid-19).

Kituo cha Marekani cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) kilitangaza kwamba watu ambao wamepewa chanjo kamili dhidi ya Covid-19 hawahitaji kufuata sheria za kuvaa barakoa wala kuzingatia masafa baina watu, isipokuwa katika hali maalum.

Baada ya uamuzi huo, maseneta wa Republican katika Baraza la Wawakilishi walivua barakoa zao na kusherehekea. Maseneta walivua barakoa zao na kusema "Karibu uhuru" huku wakipiga makofi.

Kulingana na kituo cha CDC, zaidi ya watu milioni 153 huko Marekani walipokea dozi ya kwanza na zaidi ya watu milioni 117 walipokea dozi ya pili ya chanjo ya Covid-19.Habari Zinazohusiana