UN yalaani shambulizi Iraq

Shambulizi la DAESH Iraq

1637987
UN yalaani shambulizi Iraq

Umoja wa Mataifa (UN) umetangaza kuwa uhalifu uliofanywa na kundi la kigaidi la DAESH dhidi ya jamii ya Wayazidi nchini Iraq ni mauaji ya kimbari.

Mkuu wa ujumbe wa UN, Karim Khan, ambaye alichunguza uhalifu wa kundi la kigaidi la DAESH nchini Iraq, amewasilisha ripoti yake ya 6 kwa Baraza la Usalama la UN.

Akiripoti  kuwa wamekusanya ushahidi na ushuhuda, ushahidi wa kiuchunguzi kutoka kwa makaburi ya watu na data za dijiti kutoka kwenye gari za Daesh, Khan amesema kuwa timu ya uchunguzi imepata ushahidi wazi na wa kuridhisha kwamba DAESH ilifanya mauaji ya kimbari dhidi ya Wayazidi katika mkoa wa Sinjar wa Iraq.

Timu ya UN imetambua wanachama 1,444 wa DAESH ambao walifanya uhalifu wa mauaji ya kimbari dhidi ya WaYazidi hadi sasa.

Mnamo tarehe 3 Agosti 2014, DAESH ilishambulia mkoa wa Sinjar, ambapo Wayazidi waliishi kwa wingi, na kuaa idadi kubwa ya Wazazi, na kuwakamta wanawake na wasichana.


Tagi: #UN , #DAESH , #Iraq

Habari Zinazohusiana