Idadi ya Wapalestina waliopoteza maisha yaongezeka

Idadi ya Wapalestina waliopoteza maisha katika mashambulizi ya Israel

1637980
Idadi ya Wapalestina waliopoteza maisha yaongezeka

 Idadi ya Wapalestina waliopoteza maisha katika mashambulizi ya Israel huko Gaza imeongezeka hadi 25 na waliojeruhiwa wanazidi mia moja.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya huko Gaza, upotezaji wa maisha umeongezeka hadi 25 kama matokeo ya vifo 4 zaidi baada ya mashambulizi ya hivi karibuni.

Afisa kutoka timu za Ulinzi wa Kiraia amesema kuwa upotezaji wa maisha katika mashambulizi ya hivi karibuni umetokea katika nyumba magharibi mwa Gaza, na kwamba mmoja ya waliopoteza maisha katika kaya hiyo alikuwa mwanamke na mwingine alikuwa mlemavu .

Jumatatu usiku, jeshi la Israel lilitangaza kuwa operesheni ya kijeshi ilizinduliwa katika Ukanda wa Gaza, shambulizi la anga lilifanywa huko Gaza, na idadi kubwa ya roketi zilirushwa katika eneo hilo.

Kwa upande mwingine, Rais wa Palestina Mahmud Abbas ameamua kufuta sherehe za Eid al-Fitr na kushusha bendera nusu mlingoti kwa sababu ya wale waliopoteza maisha katika shambulizi la Israel dhidi ya Gaza.Habari Zinazohusiana