Marekani na Mexico zajadili suala la uhamiaji

Viongozi wa Marekani na Mexico wakubaliana kuanzisha ushirikiano juu ya suala la uhamiaji

1636586
Marekani na Mexico zajadili suala la uhamiaji

Makamu wa Rais wa Marekani (USA) Kamala Harris na Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez Obrador, walikubaliana kuanzisha ushirikiano wa kimkakati juu ya suala la uhamiaji.

Kamala Harris, ambaye aliagizwa na Rais wa Marekani Joe Biden kushughulikia shida ya uhamiaji katika mpaka wa Mexico, alifanya mkutano mtandaoni na Rais wa Mexico Obrador.

Sababu kuu za kuingia kwa wahamiaji Marekani kutoka nchi za Amerika ya Kati zilijadiliwa kwenye mkutano.

Katika mkutano huo, ambapo hali ya uchumi ya Mexico, Guatemala, Honduras na El Salvador, inayojulikana kama "The Northern Triangle", ilijadiliwa na ikakubaliwa kuanzisha ushirikiano wa kimkakati kati ya Marekani na Mexico kwa ufurikaji wa wahamiaji kutoka nchi 3.

Wakati wa mkutano huo, pia ilielezwa kuwa juhudi za pamoja zinapaswa kufanywa ili kuhakikisha usalama katika mpaka wa Mexico na Marekani, wakati Obrador alisisitiza kwamba Harris atatarajia ziara yake nchini Mexico tarehe 8 Juni.Habari Zinazohusiana