Wagonjwa 2 wafariki hospitalini baada ya umeme kukatika

Kukatika kwa umeme kwasababisha vifo vya wagonjwa 2 wa Covid-19 kufariki hospitalini Uholanzi

1632446
Wagonjwa 2 wafariki hospitalini baada ya umeme kukatika

Wagonjwa  2 wa corona (Covid-19) waliokuwa wameunganishwa na kifaa cha oksijeni walifariki kama matokeo ya kukatika kwa umeme katika Hospitali ya Kitivo cha Matibabu cha Maastricht nchini Uholanzi.

Katika taarifa za vyombo vya habari vya ndani ya nchi, iliarifiwa kwamba Wakaguzi wa Wizara ya Afya walianzisha uchunguzi juu ya vifo vilivyothibitishwa na msemaji wa hospitali hiyo.

Mpwa wa mmoja wa wagonjwa waliopoteza maisha alitoa taarifa na kusema,

"Tulimlaza mjomba wangu Jumatatu na hali yake ilikuwa inazidi kuimarika. Ghafla habari za kifo zilitufika. Alifariki kutokana na kukatika kwa umeme."

Haijulikani ni kwanini usambazaji wa umeme wa dharura, ambao unapaswa kuamilishwa haufanyi kazi.

Kutokana na hitilafu hiyo, hali ya wagonjwa wawili wa kiume wa Covid-19 wenye umri wa miaka 76 na 67, waliounganishwa na kifaa cha oksijeni,ilizidi kuwa mbaya na wote wawili walifariki ndani ya muda mfupi.Habari Zinazohusiana