Makabiliano ya jeshi yaendelea Myanmar

Watu 9 zaidi wafariki kutokana na makabiliano ya silaha ya vikosi vya usalama nchini Myanmar

1631674
Makabiliano ya jeshi yaendelea Myanmar

Idadi ya vifo kutokana na makabiliano ya silaha ya vikosi vya usalama wakati wa maandamano ya kupinga mapinduzi nchini Myanmar iliongezeka hadi 759.

Licha ya uamuzi wa kukomesha vurugu haraka iwezekanavyo huko Myanmar, uliochukuliwa katika mkutano wa Chama cha Mataifa ya Kusini Mashariki mwa Asia (ASEAN), watu 9 zaidi waliuawa.

Katika ripoti ya kila siku iliyochapishwa na Shirika la Misaada la Wafungwa wa Kisiasa (AAPP), ilitangazwa kuwa majeruhi wengine 3 nchini wamethibitishwa ndani ya masaa 24 yaliyopita.

Wakati jumla ya watu waliopoteza maisha ilisasishwa na kuwa 759, ilirekodiwa kuwa watu 3,461 walizuiliwa.

Vile vile, Ilielezwa kuwa amri ya kuwekwa kizuizini kwa watu 1,276 bado inaendelea.

Katika mkutano wa viongozi wa ASEAN uliofanyika Indonesia mnamo Aprili 24, uamuzi wa kukomesha vurugu haraka iwezekanavyo nchini Myanmar ulichukuliwa.

Kulingana na data ya AAPP, watu 9 zaidi wameuawa nchini Myanmar kutokana na makabiliano ya kijeshi  katika maandamano ya kupinga mapinduzi tangu mkutano wa ASEAN kufanyika.Habari Zinazohusiana