Mapigano mpakani mwa Kyrgyzstan na Tajikistan

13 wafariki, 165 wajeruhiwa kwenye mapigano katika mpaka wa Kyrgyzstan na Tajikistan

1631640
Mapigano mpakani mwa Kyrgyzstan na Tajikistan

Watu wasiopungua 13 walifariki na wengine 165 walijeruhiwa kwenye mapigano ya silaha yaliyozuka kutokana na udhibiti wa mtandao wa usambazaji wa maji kwenye mpaka wa Kyrgyzstan na Tajikistan.

Mapigano hayo yalianza siku ya Jumatano baada ya kamera ya uchunguzi kuwekwa kwenye ukingo wa maji mpakani.

Ingawa pande zote zilikubaliana juu ya kusitisha mapigano na kuondoa wanajeshi, mapigano hayo yaliendelea.

Wakati Kyrgyzstan ikitangaza idadi ya watu waliopoteza maisha, takwimu juu ya idadi kwa upande wa Tajikistan bado haijulikani.

Kwa upande mwingine, Rais wa Kyrgyzstan Sadır Caparov alitoa taarifa kwenye mitandao ya kijamii na kusema,

"Ninawahimiza wakaazi wote wa Kyrgyzstan, vikundi vya kisiasa na vyombo vya habari, kuwa watulivu, wasizingatie uchochezi, wasichochee uhasama na kutokubaliana."

Kwa kuongezea, ilibainika kuwa karibu raia 800 wa Kyrgyzstan katika mkoa huo walihamishwa kwenda eneo salama.Habari Zinazohusiana