Ziara ya kwanza ya Biden ya kimataifa

Rais wa Marekani Joe Biden atatekeleza ziara yake ya kwanza ya nje ya nchi mwezi Juni

1627455
Ziara ya kwanza ya Biden ya kimataifa

Rais wa Marekani (USA) Joe Biden atafanya ziara yake ya kwanza nje ya nchi huko Uingereza na Ubelgiji mwezi Juni.

Msemaji wa White House Jen Psaki alisema katika taarifa yake kwamba Biden, ambaye alichukua madaraka mnamo Januari 20, atahudhuria Mkutano wa Viongozi wa G7 utakaofanyika Cornwall, Uingereza kati ya tarehe 11-13 Juni, kama sehemu ya ziara yake ya kwanza nje ya nchi.

Psaki alisema,

"Biden atagusia masuala ya kujitolea kwake kwa pande nyingi, vipaumbele vya sera za Marekani juu ya afya ya umma, ahadi zake za kufufua uchumi, pamoja na kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa. Pia atagusia mshikamano na maadili ya pamoja kati ya demokrasia kuu."

Psaki alibainisha kuwa Biden atafanya mikutano ya pande mbili na viongozi wa G7, pamoja na Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson, kama sehemu ya ziara yake ya Uingereza.

Akibainisha kwamba Biden atakwenda Brussels, mji mkuu wa Ubelgiji kwa ajili ya mkutano wa NATO utakaofanyika  Juni 14, baada ya Uingereza, Psaki alisema,

"Biden atathibitisha kujitolea kwa Marekani kwa muungano wa NATO, usalama wa kanda ya Transatlantic na shughuli za ulinzi wa pamoja." Psaki aliongezea kusema kuwa Biden pia atahudhuria mkutano wa Marekani na EU huko Brussels na kufanya mazungumzo ya pande mbili.Habari Zinazohusiana