Diaz-Canel achukuwa nafasi ya Castro Cuba

Rais wa Cuba Miguel Diaz-Canel ateuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha Cuba

1625034
Diaz-Canel achukuwa nafasi ya Castro Cuba

Rais wa Cuba Miguel Diaz-Canel, ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha Cuba.

Chama cha Kikomunisti cha Cuba kilitangaza kuwa Diaz-Canel mwenye umri wa miaka 61, aliteuliwa kuwa kama Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha Cuba baada ya kaka wa Rais wa zamani Fidel Castro, Raul Castro, kujiuzulu kutoka wadhifa wake wa chama hicho.

Katika taarifa hiyo, ilisisitizwa kuwa jukumu hili muhimu liliongezwa kwa jina la "Rais" alilochukuwa mnamo 2018, ambalo washiriki wa chama walimchagua Diaz-Canel kama Katibu Mkuu mpya katika Kongamano la 8.

Raul Castro alijiuzulu kutoka wadhifa wake wa Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha Cuba mnamo Aprili 16.

Castro alikuwa amewahi kusema hapo awali kuwa anataka kuacha kazi ili kutoa nafasi kwa kizazi kipya cha viongozi.Habari Zinazohusiana