Shambulizi la makombora Iraq

Kituo cha Anga cha Jeshi la Utawala wa mkoa chashambuliwa kwa makombora nchini Iraq

1623731
Shambulizi la makombora Iraq

Watu 2 walijeruhiwa katika shambulizi la makombora lililotekelezwa kwenye Kituo cha Anga cha Jeshi la Utwala wa mkoa wa Salahaddin nchini Iraq.

Kulingana na taarifa za shirika rasmi la habari la Iraq, makombora 2 yalianguka ndani ya Kituo cha Anga cha Jeshi la Utawala wa mkoa.

Watu 2 walijeruhiwa kutokana na shambulizi hilo.

Ripoti hiyo haikujumuisha habari kwamba waliojeruhiwa katika shambulizi hilo walikuwa raia au wanajeshi.

Vikosi vya muungano vinavyoongozwa na Marekani (USA) vilikuwa vimekabidhi Kituo cha Anga cha Jeshi la Utawala wa mkoa kwa jeshi la Iraq.

Inajulikana kuwa kuna wafanyikazi wa kampuni ya usalama ya Marekani ya Sallyport Global katika Kituo cha Anga.Habari Zinazohusiana