Navalny kupelekwa hospitalini

Alexei Navalny

1624159
Navalny kupelekwa hospitalini

Imeelezwa kuwa kiongozi wa upinzani nchini Urusi Alexei Navalny, ambaye alianza mgomo wa njaa akiwa gerezani, atapelekwa hospitali.

Taarifa kutoka kwa Huduma ya Kifungo ya Urusi imesema kwamba, "Iliamuliwa kuwa Navalniy atahamishiwa  hospitali iliyotengwa kwa ajili ya wafungwa katika mkoa wa Vladimir."

Katika taarifa hiyo, imesemekana kwamba Navalny alikuwa akichunguzwa kila siku na hali yake ya kiafya ilikuwa ya kuridhisha.

Mnamo Februari 2, Mahakama ya Jiji la Moscow ilibadilisha kifungo cha Navalny cha miaka 3.5 kilichosimamishwa, ambacho kilitolewa zamani kama matokeo ya kesi ya ufisadi, kuwa miaka 2.5 ya kifungo cha kawaida kwa kuhesabu adhabu aliyotumikia nyumbani.

Navalny alitangaza mnamo Machi 31 kwamba alianza mgomo wa njaa, baada ya kukataliwa ombi lake la kupewa matibabu katika gereza alilokuwa. Timu ya Navalniy ilionya kuwa kulingana na ripoti ya afya, Navalniy anaweza kupoteza maisha hivi karibuni.Habari Zinazohusiana