Johnson aahirisha safari yake India

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ametangaza kwamba ameahirisha ziara yake nchini India

1624220
Johnson aahirisha safari yake India

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ametangaza kwamba ameahirisha  ziara yake nchini India aliyopaswa kufanya mnamo Aprili 26, ambapo kumekuwa na ongezeko kubwa la maambukizi ya corona.

 Akizungumza na vyombo vya habari vya Uingereza, Johnson alisema kuwa "jambo la busara " ni kuacha ziara hiyo yenye utata nchini India, na kwamba atafanya mkutano mtandaoni na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi.

Akielezea hatua ya kuahirisha ziara hiyo, Johnson alisema ni jambo la kukasirisha.

"Mimi na Modi kwa huzuni tulifikia hitimisho kwamba siwezi kusafiri." alisema Johnson. 

"Kuzingatia kile kilichotokea India na hali ya hivi karibuni ya janga huko, nadhani ni busara kuchelewesha." aliongezea.Habari Zinazohusiana