Ajali ya ndege nchini Ufaransa

Watu wanne walipoteza maisha kutokana na ajali ya ndege

1624199
Ajali ya ndege nchini Ufaransa

Watu wanne walipoteza maisha kutokana na ajali ya ndege ndogo iliyokuwa imebeba watalii jijini Paris, mji mkuu wa Ufaransa.

Imeelezwa kuwa harufu kali ya mafuta ya taa iligunduliwa katika uchunguzi wa kwanza wa wafanyikazi wa moto katika eneo la ajali.

Ndege ndogo ya Robin DR400 ilianguka katika mji wa Saint-Pathus.

Mamlaka yameripoti kuwa watu 4, mmoja wao alikuwa rubani, wamefariki katika ajali hiyo.

Katika taarifa iliyotolewa na Kituo cha Polisi cha Beauvais, imesemekana kuwa watu watatu kwenye ndege ndogo ya mafunzo ya Robin DR400 walikuwa watalii, wakati ndege hiyo ilipokuwa ikielekea Pas-de-Calais.

Uchunguzi umeanzishwa kuhusu ajali hiyo.


Tagi: #ndege , #ajali

Habari Zinazohusiana