Shambulizi la silaha Marekani

Watu 8 wafariki kwenye tukio la ufyatulianaji wa risasi Indianapolis Marekani

1622653
Shambulizi la silaha Marekani

Watu 8 wameripotiwa kupoteza maisha kwenye tukio la ufyatulianaji wa risasi lililotokea katika taasisi ya kampuni ya FedEx, ambayo inahusika na huduma ya usafirishaji wa mizigo na shehena, katika mji wa Indianapolis nchini Marekani (USA).

Katika taasisi hiyo iliyoko karibu na Uwanja wa Ndege wa Indianapolis, mtu mmoja mwenye bunduki alifyatua risasi kiholela na kusababisha watu 4 kujeruhiwa.

Hakuna taarifa yoyote iliyotolewa kuhusu chanzo cha tukio hilo ambapo mshambuliaji pia alijiua.

Katika taarifa za waandishi wa habari wa eneo hilo, mashuhuda wa tukio walisema kwamba walimwona mshambuliaji huyo, ambaye alitakiwa kufanya kazi katika taasisi akifyatua risasi kwa bunduki ndogo aliyoishika mkononi mwake.

Na katika taarifa iliyotolewa na kampuni juu ya tukio hilo iliandikwa,

"Tuna taarifa kuhusu tukio la kusikitisha la ufyatulianaji wa risasi katika taasisi ya FedEx iliyoko karibu na Uwanja wa Ndege wa Indianapolis. Usalama ndio kipaumbele chetu. Masikitiko yetu ni kwa kila mtu aliyeathiriwa na tukio hili."Habari Zinazohusiana