Shambulizi la bomu Afghanistan

Watu 4 wafariki kwenye mlipuko wa bomu uliotokea nchini Afghanistan

1622680
Shambulizi la bomu Afghanistan

Watu 4 walifariki kutokana na mlipuko wa bomu uliotokea kando ya barabara katika mkoa wa Kandahar kusini mwa Afghanistan.

Msemaji wa Idara ya Polisi ya Kandahar Jamal Nasir Barikzey alisema kuwa bomu lililokuwa limetegwa kando ya barabara, lililipuliwa katika wilaya ya Shahwali Kot mkoani Kandahar.

Akibainisha kuwa raia 4, pamoja na watoto, walipoteza maisha kwenye shambulizi hilo, Barikzey aliwalaumu Taliban kwa tukio hilo.

Hakuna mtu yeyote aliyedai kuhusika na shambulizi hilo.Habari Zinazohusiana