Shambulizi la silaha Afghanistan

Wanajeshi 5 wauawa kwenye shambulizi la silaha lililoendeshwa na wanamgambo wa Taliban

1620737
Shambulizi la silaha Afghanistan

Wanajeshi 5 wameuawa katika shambulizi la silaha lililoendeshwa na wanamgambo wa Taliban kwenye kituo cha jeshi katika mkoa wa Balkh kaskazini mwa Afghanistan.

Msemaji wa Kituo cha 209 cha Shakin Corps, Muhammed Hanif Rizai, alisema kuwa wanamgambo hao walitekeleza shambulizi la silaha kwenye kituo cha jeshi katika mkoa wa Serasyab wilayani Chimtal, mkoa wa Balkh.

Akibainisha kuwa wanajeshi 5 waliuawa na wengine 2 walijeruhiwa katika shambulizi hilo, Rizai alisisitiza kuwa wanamgambo 7 waliuawa katika mapigano yaliyoibuka baada ya shambulizi.

Mashuhuda wa tukio walidai kuwa wanajeshi 10 walifariki kwenye shambulizi hilo na wengine 5 walikamatwa na wanamgambo hao.

Katika taarifa iliyotolewa na Taliban, ilidaiwa kuwa wanajeshi 11 waliuawa katika shambulizi hilo.Habari Zinazohusiana