Urusi yatoa onyo kwa Marekani

Serikali ya Urusi yaionya Marekani kukaa mbali na mzozo wa Crimea

1620335
Urusi yatoa onyo kwa Marekani

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Ryabkov, alionya Marekani (USA) kukaa mbali na mzozo wa Urusi na Crimea.

Katika kipindi hiki wakati mvutano unapoongezeka kwenye mpaka wa Ukraine na Urusi, meli 2 za kivita za Marekani zinatarajiwa kupelekwa Bahari Nyeusi.

Ryabkov alielezea hatua hiyo kuwa kama "uchochezi" na kusema,

''Meli za Marekani haziwezi kufanya chochote katika maeneo ya karibu na pwani zetu., huu ni uchochezi wa wazi. Wanajaribu nguvu yetu, wanachezea hisia zetu. Hawawezi kufaulu.''

Akisema kuwa kuna hatari kubwa sana ya tukio hilo, Ryabkov alionya Marekani kukaa mbali na Urusi na Crimea.

Afisa huyo wa Urusi alisema kuwa Moscow inalinda na itaendelea kuwalinda wakaazi wa Donbas.Habari Zinazohusiana