Ajali katika taasisi ya nyuklia Iran

Kituo cha nyuklia chakumbwa na ajali kwenye mtandao wa usambazaji umeme nchini Iran

1618940
Ajali katika taasisi ya nyuklia Iran

Msemaji wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran Behruz Kemalvendi, aliripoti kuwa ajali ilitokea katika mtandao wa usambazaji umeme kwenye Kiwanda cha Nyuklia cha Natanz huko Isfahan.

Kemalvendi alisema kuwa hakuna mtu aliyejeruhiwa wala hakukuwa na uchafuzi wa mazingira, na kwamba uchunguzi kuhusu chanzo cha tukio hilo unaendelea.

Mnamo Julai 2020, kulikuwa na mkasa wa moto uliozuka katika Kituo cha Nyuklia cha Natanz huko Isfahan, Iran, na madai yalitolewa kwamba lilikuwa ni shambulizi la Israel.

Mlolongo wa centrifuge wa IR6, ulio na vitengo 146 ambavyo vitatoa urani mara 10 zaidi ikilinganishwa na centrifuges zilizopita, ulianza kutumika kwa agizo la Rais Hassan Rouhani hapo jana katika kituo hicho.Habari Zinazohusiana