Miaka 4 gerezani kwa mtuhumiwa aliyewapa watu sumu

Mtuhumiwa aliyewapa sumu watu wasio na makazi ahukumiwa kifungo cha miaka 4 gerezani nchini Marekani

1618557
Miaka 4 gerezani kwa mtuhumiwa aliyewapa watu sumu

Mtuhumiwa mmoja aliyewatilia sumu watu 8 wasio na makazi na kuwarekodi video katika jimbo la California nchini Marekani (USA), amehukumiwa kifungo cha miaka 4 gerezani na mahakama ya serikali.

Ilibainika kuwa mtuhumiwa William Cable mwenye umri wa miaka 38, alichanganya madini ya sumu yanayoitwa "oleoresin capsicum", ambayo hutumiwa katika utengenezaji wa gezi za machozi, na kuwatilia watu hao kwenye vyakula.

Cable alitoa vinywaji na vyakula vyenye mchanganyiko wa sumu kwa watu 8 wasio na makazi. Pia aliwapiga picha na kurekodi video waathiriwa hao ambao walipata matatizo ya kupumua na kukumbwa na maumivu ya kinywa na matumbo.

Mahakama ya serikali iliyoko San Andreas, Kaskazini mwa California, ilimhukumu Cable kifungo cha miaka 4 gerezani kwa kukutwa na hatia ya kuwapa sumu watu wasio na makazi.Habari Zinazohusiana