Msikiti wa Pantin kufunguliwa tena Ufaransa

Msikiti wa Pantin uliokuwa umefungwa kwa muda wa miezi 6 nchini Ufaransa kufunguliwa tena Aprili 9

1616695
Msikiti wa Pantin kufunguliwa tena Ufaransa

Msikiti wa Pantin,  uliokuwa umefungwa baada ya mauaji ya mwalimu Samuel Patty nchini Ufaransa, utafunguliwa tena tarehe 9 Aprili.

Katika taarifa iliyotolewa na Gavana wa Seine-Saint-Denis, ilielezwa kuwa Msikiti wa Pantin utafunguliwa kuanzia siku ya Ijumaa, kufuatia mazungumzo na mabadiliko ya usimamizi wa msikiti yaliyofanyika.

Serikali ya Ufaransa iliamua kufunga msikiti huo kwa muda wa miezi 6 kwa madai kwamba msimamizi wa Msikiti wa Pantin huko Seine-Saint-Denis jijini Paris, alichapisha picha ya majibu yake kwa mwalimu aliyeuawa mnamo Oktoba 16 baada ya kuonyesha wanafunzi wake michoro ya kumtukana Nabii Mohammed darasani.

Uamuzi huo uliopingwa na utawala wa msikiti uliungwa mkono naMahakama ya Utawala ya Montreuil na Baraza la Nchi.Habari Zinazohusiana