EMA: ''Kuna uhusiano kati ya chanjo ya AstraZeneca na kuganda kwa damu''

EMA yatangaza uwepo wa uhusiano kati ya chanjo ya AstraZeneca na tatizo la kuganda kwa damu

1616144
EMA: ''Kuna uhusiano kati ya chanjo ya AstraZeneca na kuganda kwa damu''

Shirika la Dawa barani Ulaya (EMA), lilitangaza uwepo wa uhusiano kati ya chanjo ya AstraZeneca na tatizo la kuganda kwa damu, ingawa chanzo bado hakijafafanuliwa.

Mkuu wa Masuala ya Kibiolojia na Mkakati wa Chanjo wa EMA Marco Cavaleri, alitoa maelezo kwenye gazeti la Italia Il Messaggero na kusema kuwa kuna uhusiano kati ya chanjo ya AstraZeneca na tatizo la kuganda kwa damu.

Cavaleri alisema,

"Ni wazi kuwa kuna uhusiano na chanjo. Lakini bado hatujui chanzo kinachosababisha athari hii."

Akibainisha kwa kuelezea, "Tunajaribu kupata picha sahihi ya kile kinachoendelea ili kuelezea kwa kina ugonjwa huu unaosababishwa na chanjo," Cavaleri aliongezea kusema,

"Kuna visa vingi vya kuganda kwa damu zaidi kati ya vijana waliofanyiwa chanjo kuliko tulivyotarajia."

Kesi za kuganda kwa damu ambazo ziliongezeka kama matokeo ya matumizi ya chanjo ya AstraZeneca katika nchi za Ulaya zilisababisha hofu ya kiafya na kuanza kuhoji usalama wa chanjo.

Hata hivyo, nchi zingine ikiwa ni pamoja na Italia, zilitangaza kuwa "faida zake zinazidi hatari na zinapaswa kuendelea kutumika."Habari Zinazohusiana