Ziara ya kwanza ya Draghi nchini Libya

Waziri Mkuu wa Italia Mario Draghi akutana na Waziri Mkuu wa Libya Abdulhamid Dbeibeh mjini Tripoli

1615924
Ziara ya kwanza ya Draghi nchini Libya

Waziri Mkuu wa Italia Mario Draghi alikutana na Waziri Mkuu wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa wa Libya Abdulhamid Dbeibeh wakati wa ziara yake nchini humo.

Dbeibeh alimkaribisha Draghi kwa sherehe rasmi katika makao makuu ya waziri mkuu. Viongozi hao wawili walifanya mkutano wa pamoja na waandishi wa habari baada ya mikutano kati ya wajumbe.

Katika hotuba yake, Dbeibeh alisema kuwa wanaona umuhimu wa kuimarisha ushirikiano wa kimkakati kati ya Libya na Italia.

Akibainisha kuwa walikubaliana juu ya umuhimu wa kutia saini makubaliano ya ushirikiano na kuanza safari za ndege kati ya nchi hizo mbili, Dbeibeh alisema kwamba pia walikubaliana kuwezesha taratibu za raia wa Libya katika suala la kupata visa za kuingia Italia.

Akifahamisha kuwa walikubaliana kubadilishana maoni katika uwanja wa nishati na umeme, Dbeibeh alielezea ukweli kwamba kampuni kubwa ya mafuta ya Italia ya "Eni" ni "muhimu sana kwa uchumi wa nchi zote mbili".

Waziri Mkuu wa Libya alielezea kuwa nchi yake ni njia ya kupitia wahamiaji na suala la uhamiaji sio tu tatizo la nchi mbili, bali ni tatizo la Ulaya na ulimwengu mzima kwa ujumla.

Kwa upande mwingine, Waziri Mkuu wa Italia Draghi alisema kuwa baada ya kuchukua ofisi mnamo Februari 13, alifanya ziara yake ya kwanza ya kimataifa huko Tripoli na kwamba mkutano wake na mwenzake wa Libya ulikuwa "wa kusisimua sana na wa kuridhisha".Habari Zinazohusiana