Mapigano kati ya wanajeshi na waasi India

Wanajeshi 22 wapoteza maisha kwenye mapigano na waasi wa Maoist nchini India

1614513
Mapigano kati ya wanajeshi na waasi India

Katika jimbo la Chattisgarh nchini India, idadi ya wanajeshi waliouawa kwenye mapigano na waasi wa Maoist iliongezeka kutoka 5 hadi 22.

Kulingana na taarifa za vyombo vya habari vya ndani ya nchi, Mkuu wa Idara ya Polisi ya Chattisgarh, Ashok Juneja alisema kwamba wanajeshi walivamia eneo la makazi katika msitu ulioko jijini Bijapur ambapo mapigano yalizuka kati yao na waasi wa Maoist.

Akibainisha kuwa baada ya mapigano hayo, miili ya wanajeshi 17 ilipatikana na kupelekea idadi ya wanajeshi waliopoteza maisha kuongezeka hadi 22, Juneja pia alitangaza kujeruhiwa kwa wanajeshi 32.

Juneja aliongezea kusema kuwa waasi 15 waliuawa katika mapigano hayo.

Mamlaka ilitangaza jana kuwa wanajeshi 5 waliuawa na wengine  12 walijeruhiwa katika mapigano hayo yaliyodumu kwa masaa 4.

Wakiongozwa na kiongozi wa mapinduzi wa China Mao Zedong, waasi wa Maoist wamekuwa wakipanga mashambulizi ya silaha katika majimbo mengi ya kaskazini, mashariki na katikati mwa India tangu mwaka 1967.Habari Zinazohusiana