Mvutano kwenye maandamano Uingereza

Wananchi wa Uingereza waandamana kupinga sheria inyaowapa polisi mamlaka zaidi ya makabiliano

1614367
Mvutano kwenye maandamano Uingereza

Mvutano mkubwa ulizuka kati ya polisi na wanaharakati wakati wa maandamano dhidi ya rasimu ya sheria ambayo iliwapa polisi mamlaka zaidi ya kuingilia kati maandamano katika mji mkuu wa London nchini Uingereza.

Maelfu ya waandamanaji kutoka vikundi tofauti walikusanyika eneo la Hyde Park kupinga muswada huo na wakaandamana hadi Uwanja wa Bunge.

Waandamanaji hao, wakiwa wamebeba mabango yaliyoandikwa  "Hakuna mamlaka tena kwa polisi", "Lindeni haki zetu" na "Hatutanyamaza", walidai rasimu hiyo ifutiliwe mbali.

Wakati wa hotuba katika uwanja wa Bunge, kikundi kimoja cha waandamanaji kilifunga barabara na kuzuia lori kupita.

Papo hapo maafisa wa polisi waliingilia kati na kukabiliana na waandamanaji.

Polisi walianza kutupia vitu na waandamanaji na kusababisha rabsha kuzuka.

Baada ya makabiliano ya muda mrefu, baadhi ya waandamanaji walikamatwa wakati lori lilipopata njia ya kupita.

Baada ya kuingilia kati, waandamanaji wapatao 300 walikwenda katika Trafalgar Square na kufunga barabara na kusababisha msongamano.

Polisi waliingilia kati ten ana kuwazuia  waandamanaji wengi.

Wakati wale waliovuka utepe wa polisi wakiendelea na maandamano yao, ilionekana kuwa wanaharakati wengine walitupa makopo ya takataka barabarani na kuzuia magari kupita.

Kutokana na kukabiliwa na polisi kwa mara nyingine tena, waandamanaji wengi walitoroka kwa kukimbilia kwenye vichochoro vya barabara za mitaa.

Taarifa iliyotolewa na polisi, iliarifu kuwa watu 26 walizuiliwa hadi saa 20.45 (TSI 22.45) na idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka.

Katika taarifa hiyo, ilitangazwa kuwa maafisa 10 wa polisi walijeruhiwa kidogo.Habari Zinazohusiana