Kesi ya George Floyd yaanza Marekani

Jopo la majaji laanza kusikiza kesi ya afisa wa polisi anayeshtakiwa kwa mauaji ya George Floyd nchini Marekani

1611435
Kesi ya George Floyd yaanza Marekani

Kesi ya afisa wa polisi wa zamani Derek Chauvin, ambaye alisababisha kifo cha George Floyd raia mwenye asili ya Kiafrika kwa kushinikiza goti lake shingoni wakati wa kumkata katika jimbo la Minnesota nchini Marekani imeanza.

Kwa mara ya kwanza, afisa wa polisi wa zamani Derek Chauvin alifika mbele ya mahakama.

Majaji 15 wanaojumuisha watu 9 weupe, 6 wenye asili ya Kiafrika na makabila mengine, walichaguliwa kwenye jopo la kusimamia kesi hiyo.

Majaji walionyeshwa video iliyoonyesha afisa wa polisi alipokuwa akimbana shingo ya Floyd wakati wa kumkata.

Kesi hiyo inakadiriwa kuchukua takriban mwezi mmoja.

Wakati wa kesi hiyo, hatua kubwa za usalama zilichukuliwa dhidi ya maandamano ya wafuasi wa Floyd huko Minneapolis.

Imeelezwa kuwa endapo afisa huyo wa polisi atapatikana na hatia katika kesi hiyo ambapo inamkabili kwa mauaji, ataweza kuhukumiwa kifungo cha hadi miaka 40 gerezani.

Walakini, mawakili wanasema kuwa hakuna mifano ya maafisa wa polisi waliopatikana na hatia katika kesi ambazo zinawakibili kwa "mauaji ya raia" nchini Marekani.

Floyd mwenye umri wa miaka 46, alizuiliwa huko Minneapolis, Minnesota, kwa tuhuma za udanganyifu mnamo Mei 25, 2020, ambapo afisa wa polisi mwenye umri wa miaka 44 Derek Chauvin alimbana kwa kumwekea goti shingoni licha kumwambia kuwa "hawezi kupumua" kwa dakika 9.Habari Zinazohusiana