Wahamiaji wakita kambi mjini Paris

Wahamiaji waweka kambi katika mji mkuu wa Paris na kutoa wito kwa serikali ya Ufaransa

1609162
Wahamiaji wakita kambi mjini Paris

Wahamiaji wa kiholela walikita kambi katika mji mkuu wa Paris nchini Ufaransa  ili kupaza sauti zao kwa serikali kuhusu hali mbaya waliyokuwa nayo.

Kama sehemu ya "usiku wa mshikamano", wahamiaji wengi wanaojumuisha Waafghanistan, watoto na wanawake, waliweka kambi katika Uwanja wa Republique Square chini ya uongozi wa vyama mbalimbali na kutoa wito kwa serikali.

Reza Jafari,  Rais wa Chama cha Watoto wa Afghanistan na mshiriki wa kikundi cha "Requisitions" ambacho hufanya kazi kwa wahamiaji wa kiholela, alisema,

"Wahamiaji, pamoja na vyama, walichukua hatua hii kudhihirisha wazi hali yao ionekane Paris. (Mkuu wa Polisi wa Paris) Didier Lallement amekataza wahamiaji kujenga mahema Paris, kwa hivyo wameweza kuweka mahema karibu na Paris. Usiku wa leo tulitaka kudhihirisha wazi hali isiyoonekana."

Akibainisha kuwa usiku huo ulikuwa wa mshikamano, Jafari alisema kuwa Manispaa ya Paris inafanya utafiti ili kujua idadi ya watu wanaoishi mitaani, hivyo basi wameweka kambi katika uwanja huo ili kuwarahisishia kazi zao.

Akikumbusha kwamba wahamiaji waliweka kambi katika uwanja huu mnamo Novemba 2020, Jafari pia alisema,

"Ilikuwa mbaya sana na ilisababisha vurugu. Wahamiaji hawa hawaogopi polisi. Kila siku wanajitahidi kuishi chini ya madaraja. Polisi wanapofika chini ya madaraja, hawasiti kuvuruga mahema na kuwapiga wahamiaji kwa kutumia marungu na gesi ya machozi."

Akifahamisha kuwa wahamiaji wanaomba hifadhi, Jafari alibaini kuwa haki ya msingi ya wahamiaji ni kuwa na mahali pa kukaa, lakini ombi hilo halijawahi kutekelezwa.

"Haikubaliki kwa familia kukaa chini ya madaraja katika ardhi ya haki za kibinadamu," Jafari alitoa maoni yake.

Usiku wa Novemba 24 huko Paris, polisi waliwafukuza karibu wakimbizi 500, haswa Waafghanistan, ambao waliweka mahema katika Uwanja wa Republique, na kuwatawanya kwa kutumia gesi ya machozi.Habari Zinazohusiana