Mkutano wa Biden na viongozi wa nchi za EU

Rais wa Marekani Joe Biden ashiriki mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya Ulaya mtandaoni

1609142
Mkutano wa Biden na viongozi wa nchi za EU

Rais wa Marekani (USA) Joe Biden, alitoa ujumbe kwa viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ulaya (EU) ili kufufua uhusiano wao na Marekani.

Katika taarifa iliyoandikwa kutoka Ikulu ya White House, iliarifiwa kwamba Biden alihudhuria mkutano wa mtandaoni ndani ya wigo wa Kikao cha Jumuiya ya Ulaya (EU).

Taarifa hiyo ilieleza kwamba mkutano huo ulioongozwa na Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel, ulihudhuriwa na viongozi wa serikali za nchi 27 za wanachama wa EU, ambapo Biden kwa mara nyingine alielezea kujitolea kwake kufufua uhusiano kati ya EU na Marekani.

Taarifa hiyo ilibainisha kuwa Biden alifahamisha EU kwamba ina nguvu kimasilahi kwa Marekani, na ikasisitiza umuhimu wa maadili ya kawaida ya kidemokrasia na ushirika mkubwa zaidi wa kibiashara na uwekezaji.

Ilielezwa kuwa Biden alitaka ushirikiano wa karibu juu ya maswala kama vile kupambana na janga la corona, kushughulikia tishio la mabadiliko ya hali ya hewa, kukuza uhusiano wa kiuchumi na demokrasia.

Mwishowe taarifa hiyo pia iliandikwa,

"Rais Biden amebainisha hamu yake ya kushirikiana na China na Urusi kwa masilahi ya pamoja ya sera za kigeni. Isitoshe, aligusia pia suala la Marekani kuendeleza mawasiliano na EU kwa ajili ya Uturuki, Caucasus Kusini, Mashariki ya Ulaya na Magharibi mwa Balkan."Habari Zinazohusiana