Shambulizi kwenye kiwanda cha marumaru Afghanistan

Wafanyakazi 7 wafariki kwenye shambulizi la silaha lililoendeshwa katika kiwanda cha marumaru nchini Afghanistan

1595170
Shambulizi kwenye kiwanda cha marumaru Afghanistan

Wafanyakazi 7 wameripotiwa kupoteza maisha kwenye shambulizi la silaha lililotekelezwa katika kiwanda cha marumaru mkoani Nangarhar mashariki mwa Afghanistan.

Mkuu wa Polisi wa Nangarhar Juma Gul Himmet alisema kuwa watu wasiojulikana walishambulia kiwanda cha marumaru kilichoko kaunti ya Surhrod.

Himmet alitangaza kuwa wafanyikazi 7 walipoteza maisha kwenye shambulizi hilo.

Nilufer Aziz ambaye ni Naibu wa Baraza la Mkoa wa Nangarhar, alibainisha kwamba wafanyikazi waliopoteza maisha katika shambulizi hilo walikuwa wanatokea jamii ya  Washia wa Hazara na wahusika wa shambulizi hilo wanaweza kuwa ni mashirika ya kigaidi.

Hakuna mtu aliyedai kuhusika na shambulizi hadi kufikia sasa.

Mashambulizi yameongezeka hivi karibuni kote nchini Afghanistan.

Asubuhi ya leo, daktari wa kike anayefanya kazi katika hospitali ya serikali ya mji wa Jalalabad mkoani Nangarhar pia alifariki kwenye shambulizi la bomu.Habari Zinazohusiana