Papa kuizuru Iraq kwa mara ya kwanza katika historia

Kwa mara ya kwanza katika historia Papa Francis atafanya ziara nchini Iraq

1594892
Papa kuizuru Iraq kwa mara ya kwanza katika historia

Kwa mara ya kwanza katika historia Papa Francis atafanya ziara nchini Iraq.

Kiongozi huyo wa Wakatoliki na Rais wa Vatican anatarajia kuelekea nchini Iraq katika ziara yake rasmi siku ya kesho.

Kulingana na mpango uliotolewa na Vatican, Papa Francis atafanya mazungumzo kwanza katika mji mkuu Baghdad wakati wa ziara yake itakayofanyika tarehe 5-8 Machi.

Mnamo Machi 6, ataelekea huko Najaf, na kukutana na  Ayatollah Ali na mamlaka ya kidini ya Washia huko Iraq.

Papa Francis atakutana na Serikali ya Mkoa wa Kikurdi wa Iraq huko Erbil mnamo Machi 7, na kisha atatembelea Mosul na kurudi Vatican mnamo Machi 8.

Wakati huo huo, Msemaji wa Vatican Matteo Bruni ametoa tamko kabla ya ziara ya Papa nchini Iraq.

Akielezea kwamba Papa anakwenda nchi ambayo idadi kubwa ya watu ni Washia, Bruni amesema kuwa kuna mahitaji tofauti ya usalama kuliko ziara zingine na akasema kwamba "Papa ana uwezekano wa kutumia magari ya kivita".

Papa alifuta ziara zake za nje mnamo 2020 kutokana na janga la corona.

Ziara ya Iraq itakuwa safari ya 33 ya nchi za nje ya Papa, ambaye hajafanya safari za nje kwa takriban miezi 16.


Tagi: #Iraq , #ziara , #Papa

Habari Zinazohusiana