Chanjo ni lazima kwa hija mwaka huu

Sharti jipya kwa wale watakaohiji mwaka huu

1593360
Chanjo ni lazima kwa hija mwaka huu

Saudi Arabia imetangaza kuwa ni sharti la msingi kupigwa chanjo dhidi ya corona kwa ajili ya kufanya hija mwaka huu.

Kulingana na gazeti la Ukaz, maafisa katika wizara ya Waziri wa Afya Tawfig Al-Rabiah wamesema kwamba ni lazima kuwa umepigwa chanjo ya Covid-19 kwa wale ambao wanataka kushiriki katika hija, na kwamba hii ni moja ya masharti ya kushiriki hija mwaka huu nchini Saudi Arabia.

Waziri Rabiah ameomba maandalizi ya mapema yafanyike kwa kuajiri wataalamu wa huduma ya afya kufanya kazi katika vituo vya afya huko Mecca, Medina na maeneo matakatifu.

Imearifiwa pia katika habari kwamba Waziri aliamuru kuundwa kwa tume ya Covid-19 kwa mahujaji.Habari Zinazohusiana