UN yalaani shinikizo dhidi ya waandamanaji Myanmar

Umoja wa Mataifa (UN) walaani ukandamizaji wa raia na shinikizo za jeshi dhidi ya waandamanaji wa Myanmar

1592562
UN yalaani shinikizo dhidi ya waandamanaji Myanmar

Umoja wa Mataifa (UN) ulilaani ukandamizaji mkali wa raia nchini Myanmar na kusema kuwa matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji wa amani hayakubaliki.

Msemaji wa Ofisi ya Katibu Mkuu wa UN Stephane Dujarric, alitoa taarifa ya maandishi kuhusu ghasia za hivi karibuni zilizoko nchini Myanmar.

Akitoa matamshi yaliyosema,"Katibu Mkuu analaani vikali ukandamizaji wa vurugu nchini Myanmar na ana wasiwasi sana kuhusu idadi kubwa ya vifo na majeruhi", Dujarric alisisitiza kuwa matumizi ya nguvu na ukamataji wa kiholela wa jeshi dhidi ya waandamanaji wa amani nchini Myanmar haikubaliki.

Dujarric aliongezea kusema, "Katibu Mkuu anatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kukusanyika pamoja na kutuma ujumbe wa wazi kwa wanajeshi kuheshimu maamuzi ya wananchi wa Myanmar."

Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa ilitangaza jana kuwa watu wasiopungua 18 walifariki kutokana na makabiliano ya vikosi vya usalama katika maandamano ya kupinga mapinduzi ya Myanmar.

Jeshi la Myanmar lilipindua serikali ya utawala mnamo Februari 1, baada ya vyama vya kisiasa vilivyo karibu nao kutoa madai ya udanganyifu katika uchaguzi wa tarehe 8 Novemba 2020.

Jeshi lilitangaza hali ya hatari kwa mwaka mmoja na kukamata maafisa wengi na viongozi wa chama tawala akiwemo Aung San Suu Kyi.Habari Zinazohusiana